Penzi Langu

Lyrics:

Eeeh Yesu Ooh Ewe Yesu Penzi langu kwako
Yesu jina lako kama asali kwenye ulimi wangu ni tamu
Yesu pendo lako kama mvua rasha rasha yanyesha ni tamu
Yesu amani yako kama maji matulivu masafi matamu

Ninakupenda nakupenda penzi langu ooh
Penzi langu ni kwako
Minakupenda nakupenda penzi langu ooh
Penzi langu ni kwako

Ukanitoa kwenye shimo la mauti
Ukaniweka karibu nawe
Kanipanguza machozi ukanitoa kwenye moto
Ili mimi nikae salama
Yesu wangu imani yangu naiweka kwako nisiabike
Maana upendo wako wanitosha wanitosha

Mie nakupenda nakupenda
Penzi langu ni kwako
Mie nakupenda nakupenda
Penzi langu ni kwako

Nakumbuka jinsi ulivyonipenda
Ukamtoa mwana wako anifie
Nisemeje ila ni shukurani kwako

Yeiyee nakupenda nakupenda
Penzi langu ni kwako ewe
Mie nakupenda nakupenda
Penzi langu ni kwako ewe Source: Penzi Langu Lyrics - TuneDem Band