Ndoa

Lyrics:

Ndoa ni mpango takatifu tangu mwanzo, 

ujumbe njema utokao kwa Baba, 

yahitajika hekima kuitunza 

hadi kifo kiwatenganishe. 


Chorus

Mke si kidude cha kujaribu miguu yako, 

Mume si kipasa sauti cha kupigia kelele

Mpendaneni, msichokozane, 

amani ya Bwana iwe ndani yenu.


2. Kazi kwenu sasa maishani mwenu, 

mdumu milele kwenye upendo wa Yesu, 

ni Mungu pekee aweza kuwalinda na kutatua 

mashaka yenu ya Maisha. 


Bridge 

Muwe mfano bora kwa watoto wenu, 

waonyeshe njia ile ya uzima ya wokovu, 

Nanyi watoto wote watiini wazazi wenu,

mibaraka yake Mungu 'tawakirimia.