Huniongoza

Lyrics:

Huniongoza Mwokozi,

ndipo nami hufurahi

Niendapo pote napo,

ataniongoza papo


Huongoza hunishika, kwa mkono wa hakika

Nitaandamana naye Kristo aniongozaye


Pengine ni mashakani,

nami pengine rahani

Ni radhi ijayo yote,

yupo nami siku zote


Huongoza hunishika, kwa mkono wa hakika

Nitaandamana naye Kristo aniongozaye


Mkono akinishika,

kamwe sitanung’unika

Atachoniletea,

ni tayari kupokea


Huongoza, hunishika kwa mkono wa hakika

Nitaandamana naye Kristu aniongozaye


Nikiishika kazi chini,

nitakwenda huko mbinguni

Nako nitamtukuza,

Kristo aliyeniongoza


Huongoza hunishika, kwa mkono wa hakika

Nitaandamana naye Kristo aniongozaye


Nitaandamana naye kristo aniongozaye 

Nitaandamana naye kristo aniongozaye

Nitaandamana naye kristo aniongozaye