Mungu Wangu

Lyrics:

Mungu wangu mbona umeniacha? 

Mbona uu mbali na kuugua kwangu Baba? 

Wote wanaoniona hunicheka 

Nakulilia nakusihi unijibu 


Najua mtetezi wangu yu hai 

Kamwe sitakata tamaa 

Aijua njia niendayo, ataniongoza milele 

Akishanijaribu nitatoka dhahabu 

Baada ya dhiki nitamwona muumba wangu 


Mashtaka yao yana uchungu mwingi 

Laiti ningefika kwa muumba wangu 

Hakika ningenena na mwenyezi Mungu 

Ningeliweka dua langu mbele yake 


Najua mtetezi wangu yu hai 

Kamwe sitakata tamaa 

Aijua njia niendayo, ataniongoza milele 

Akishanijaribu nitatoka dhahabu 

Baada ya dhiki nitamwona muumba wangu 


Hema za wapokonyi zafanikiwa baba 

Waasi nao hunawiri Bwana 

Mipango ya wenye dhambi nao hunawiri 

Basi tumaini langu liko wapi 


Najua mtetezi wangu yu hai 

Kamwe sitakata tamaa 

Aijua njia niendayo, ataniongoza milele 

Akishanijaribu nitatoka dhahabu 

Baada ya dhiki nitamwona muumba wangu