Twende Kwa Yesu

Lyrics:

Twende kwa Yesu, mimi nawe,

Njia atwonya tuijue

Imo chuoni; na mwenyewe,

Hapo asema, njoo!


Na furaha tutaiona,

Mioyo ikitakata sana,

Kwako mwokozi kuonana,

Na milele kukaa.


Wana na waje, ”atwambia.

Furahini mkisikia;

Ndiye mfalme wetu pia,

Na tumtii, njoo.


Na furaha tutaiona,

Mioyo ikitakata sana,

Kwako mwokozi kuonana,

Na milele kukaa.


Wangojeani leo yupo;

Sikiza sana asemapo;

Huruma zake zikwitapo 

Ewe kijana njoo 


Na furaha tutaiona,

Mioyo ikitakata sana,

Kwako mwokozi kuonana,

Na milele kukaa.