Jina La Yesu

Lyrics:

Hata hili linapita 

Hata hili lina mwisho 

Hata hili linapita 

Hata hili lina mwisho 


Ni kweli napitia kipindi kigumu 

Moyo wangu unauma 

Nijaribu lililosima mbele zako kizito 

Moyo unafadhaika 

Lakini namwimini Mungu atanivusha tu 

Wakati mwingine nilikumbana na hatari 

Ya kugharimu uhai wangu 

Mungu hakuniacha, MUngu alinibeba 

Hata hili linapita, Hata hili lina ukomo wake 

Kila jaribu linalokuja mbele yangu 

Bibilia linasema lina mlango wa kutokea 

Waswahili wanasema hakuna mrefu lisilokuwa na mwisho 

Hata hili lina mwisho 


Majaribu hayana budi kuyavumilia 

Nitavumilia oh sitawaza uovu 

Manabii walijaribiwa 

mitume wengine kufa kwa ajili ya kazi ya Mungu 

Nami pia sitavunjika moyo 


Vumilia vumilia vumilia jipe moyo 

Vumilia vumilia hatimaye utashinda 


Vikwazo vingi na vitisho mbele yako 

Usiogope usiogope 

Ndoa yako japo kiasi hicho 

Usiogope jibu lipo leo 

Huduma japo pigwa vita hivyo 

Usiogope jua yupo mtetezi 

Ukimwona nyani mzee 

Jua kakwepa mishale mingi 

Usiogope yupo mtetezi 

Usiogope vita ni vya Bwana 

Usiogope vita ni vya Bwana 


Sitaogopa sitaogopa 

Mungu yuko nami 

Sitaogopa sitaogopa 

Sitaogopa atanishindia 


Sitaogopa sitaogopa 

Mungu yuko nami 

Sitaogopa sitaogopa 

Sitaogopa atanishindia Jina lako Yesu lina nguvu 

Na uweza la kuvunja hila 

minyororo ya shetani 


Jina lako Yesu lina nguvu 

Na uweza la kuvunja hila 

minyororo ya shetani 


Ulisema Bwana tutatenda 

Zaidi ya uliyoyatenda 

Naomba Bwana tukiimba 

Walio wagonjwa wanapona 


Ulisema Bwana tutatenda 

Zaidi ya uliyoyatenda 

Naomba Bwana tukiimba 

Waliopotoka waokoke 


Waliokuwa huduma zao zimevunjika 

Zinarudi kusimama 

Viwete watembee visiwi wasikie ukitajwa 

Nguvu za giza zimeshindwa 

Ngome za shetani zimeshindwa 

Kwa jina lako Kwa jina lako 


Jina lako Yesu lina nguvu na uweza 

Wa kuvunja hila 

minyororo ya shetani 


Mauaji ya wake na waume zetu (shindwe) 

Chuki kati ya binadamu (shindwe) 

Unafiki na masengenyo (shindwe) 

In the mighty name of Jesus christ (shindwe) 


Every nation bow and every tongue confess 

That Jesus is the Lord yeah 

Every knee shall bow and every tongue confess 

Jesus is the Lord, Jesus the Lord 


Jina lako Yesu lina nguvu na uweza 

Wa kuvunja hila 

minyororo ya shetani 


Kila goti lipigwe kila ulimi ukiri 

Kwamba wewe ni Bwana, wewe ni Bwana